Connect with us

Biashara

Kinondoni kujengwa soko la kisasa

Published

on

Mkuu wa Wilaya  ya Kinondoni Mh, Ally Hapi amefunguka na kusema wanatarajia kujenga Soko jipya la kisasa eneo la Magomeni sokoni kwa gharama ya shilingi bilioni 9.

Mkuu huyo wa wilaya amesema “tayari Kinondoni imepokea fedha kutoka Ofisi ya Raisi Tamisemi kwa ajili ya kuanza ujenzi”

Soko hilo litakuwa na ghorofa kadhaa na litabeba wafanyabiashara wa aina zote kwa mpangilio ikiwemo huduma za fedha ,lift, na eneo la maegesho lenye uwezo wa kuegesha magari hadi 150 kwa wakati mmoja.

Soko la Machinga Complex Ilala Dar es salaam

Soko la Mwanjelwa Mbeya

Hata hivyo baadhi ya wadau walitoa maoni yao wasema ujenzi wa soko la ghorofa mara nyingi hukosa wafanyabiashara huku wakitolea mfano soko la Machinga Complex lililopo Ilala Dar es Salaam pamoja na soko la Mwanjelwa Mbeya ambayo yamejengwa kwa mfumo huo na yamekosa wapangaji.

Mh. Ally Hapi amebainisha kuwa tatizo ni mfumo  na kwamba hili soko litakuwa na huduma za soko, maduka, coffee, shops pamoja na huduma za benki.

Kukamilika kwa soko la Magomeni kutaongeza idadi ya masoko katika jiji la Dar es Salaam.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Biashara

TRA kupiga mnada makontena 20 ya Paul Makonda

Published

on

Mamlaka ya Mapato nchini(TRA), imetangaza kupiga mnada Makontena 20 yanayotajwa kuwa ni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda,
kusudio hili litatekelezwa ikiwa Makonda atashindwa kulipa ushuru na kuyachukua Makontena hayo ndani ya siku 30 kuanzia Jumatatu wiki hii.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema, bidhaa zote zinapoagizwa na kufika bandarini zinatakiwa kuondolewa ndani ya siku 90.

Kwa mujibu wa tangazo la TRA notisi ya siku 30 imetolewa kwa wateja nane akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ambao mizigo yao imekaa bandarini zaidi ya muda unaotakiwa.

 

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania