Connect with us

Maisha

Tetesi za Ukweli wa Mambo; Ndoa ya Prince Harry

Published

on

Mjukuu wa Malkia Prince Harry anatarajia kufunga ndoa na Mchumba wake Meghan Markle tarehhe 19 Mei mwaka huu.

Tangu wawili hao waweke mahusiano yao hadharani Novemba 17, kumekuwepo na minong’ono ya hapa na pale kuhusu siku yao ya harusi hatua iliyopelekea mpaka wengine kudhani kuwa mahusiano yao ni Mchezo wa kuigiza.

Prince Harry alinukuliwa akisema muda mwingi yeye na mchumba wake wamekuwa wakipanga harusi yao na wamekuwa wakitumia muda na nguvu nyingi katika hilo.

“Tumebanwa sana na mipango ya harusi, lakini tunajitahidi sana kufanya kila njia ili iwe ya kitofauti” alisema Prince Harry.

Muonekano wa kipekee wa Kadi za Mwaliko wa Harusi ya Kifalme

Taarifa zilizothibitishwa na Kensington Palace zinaeleza kuwa harusi hiyo ya kifalme itafanyika Windsor Castle na mpaka sasa watu 600 wapewa mualiko wa kuhudhuria Harusi hiyo ya Kifalme na ya aina yake.

Ndoa ya Prince Harry na Markle itafanyika kanisa la Mtakatifu George “St George’s Chapel” Windsor Castle  majira ya saa 12:00 mchana.

Malkia ametoa ruhusa ya sherehe hiyo kufanyika mahali pa ibada ambapo panakadiriwa kuchukua watu 800, na mambo ya msingi ya harusi na huduma kama muziki, maua, mapambo na mapokezi yatagharamiwa na familia ya kifalme.

Inaarifiwa wazazi wa Bibi Harusi mtarajiwa watawasili  Uingereza  wiki moja kabla ya harusi ambapo mama yake Meghan Doria Ragland ataambatana na mumewe Markel kueleka Windsor Castle mapema asubuhi.

Swali ni nani atakuwa msimamizi wa Harry yaani kwa lugha ya kizungu Bestman na nani atakuwa Msimizi wa Meghan?

Taarifa ya Kensington Palace inaeleza wazi kuwa Prince Williams ambaye ni kaka yake na Harry ndiye atakaye kuwa msimamizi na kwa upande wa Meghan kuna tetesi kuwa Millie Mackintosh ambaye anatajwa kuwa ni rafiki yake ambaye amekuwa akifurahia uwepo wake huenda akawa ndiye msimamizi.

Mrembo anayetajwa kuwa msimamizi wa Bibi Harusi

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Maisha

Ajinyonga mpaka kufariki

Published

on

Joseph Ojur mwenye umri wa 52 mkazi wa ukanda wa  Kabagu katika manispaa ya Njeru amejinyonga mpaka kufa jumapili ya June 3 baada ya kunyimwaunyumba na mkewe.

Ojur inasemekana kuwa alimwambia mkewe kuwa alifanya vipimo vya ugonjwa wa UKIMWI na akakutwa nao.

Na tangu amwambie mkewe hivyo amekuwa akinyimwa ‘unyumba’.

Kamanda wa Polisi eneo la Njeru, Christopher Tuhunde amesema kuwa, marehemu alijinyonga ndani ya nyumba yake na jeshi hilo linaendelea kuchunguza kwa undani juu ya tukio hilo ili kuja na ripoti kamili kuhusiana na kujinyonga kwa Ojur.

Hata hivyo Tuhunde amewashauri wakazi wa eneo hilo kupenda kuomba ushauri kwa wenzao juu ya matatizo yanayowakabili kuliko kukimbilia kujiua.

Continue Reading

Maisha

Je, Unaweza Kujivunia Ujauzito ukiwa na umri gani? Brigitte Nielsen ametangaza kuwa Mjamzito

Published

on

Muigizaji nyota kutoka Italia ambaye ana asili ya Dernmark na aliyewahi kuwa mke wa zamani wa Sylvester Stallone ametangaza kuwa anatarajia kuwa ana ujauzito aliopewa na mume wake wa sasa Mattia Dessi.

Brigitte Nielsen ameshangaza wengi baada ya kutangaza ujauzito huo akiwa na umri wa miaka 54, na taarifa hizo amezitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Tayari ni mama wa watoto wanne ambao ni Julian, Killian, Douglas na Raoul ambaye ndio mtoto wake wa kwanza kwa mume wake wa sasa ambaye amedumu naye kwa miaka kumi na miwili tangu walipooana mwaka 2006.

happy time ❤ positive vibes #happyness #positivevibes

A post shared by Brigitte Nielsen (@realbrigittenielsen) on

Katika moja ya picha yake inayo onyesha tumbo la mtu mjamzito, aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya laki moja aliandika “Family is getting Longer” akimanisha kuwa sasa Familia inakua.

Mwanzoni amewahi kuwa kwenye ndoa na Roul Meyer, Sebastian Copeland, Sylvester Stallone na Kasper Winding.

Continue Reading

Maisha

Kenya: Mwanafunzi aunda gari linalotumia nishati ya jua Kenya

Published

on

Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ameunda gari linalotumia kawi ya jua, gari ambalo limekuwa likiwavutia watu sana mtaani kwake, na mtandaoni.

Samuel Karumbo, 30, ni mwanafunzi katika chuo cha mafunzo anuwai cha serikali mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya lakini ameliunda gari lake katika eneo la Langas, Eldoret si mbali sana na mji wa Kitale.

Anasema gari lake, ambalo lina mitambo mitatu ya sola iliyobandikwa, linaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 kwa siku.

Mitambo hiyo inaweza kuzalisha kadri ya jumla ya watu 260.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania