Connect with us

Maisha

Fisi atenganisha ndoa ya watu

Published

on

Mkazi wa wilayani Igunga, mkoani Tabora ameuawa na fisi na mwingine kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na mnyama huyo katika Kata ya Ziba, wakati wakirejea nyumbani kutoka kwenye klabu ya pombe.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ziba,Azizi Kombe alimtaja aliyeuawa ni Mwajuma Masanja (37), mkazi wa Kijiji cha Iduguta wilayani Nzega na Shija Maneno (35), mkazi wa Kitongoji cha Ipuli Kijiji cha Igumila Kata ya Ziba ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufani Nkinga na hali yake ni mbaya.

“Watu hao walikuwa ni mtu na mpenzi wake ambao walikuwa wakinywa pombe za kienyeji kwenye klabu iliyopo Kata ya Ziba  baada ya kufika saa 3 usiku waliamua kuondoka kurudi nyumbani”

Hata hivyo, Kombe alibainisha wakati wakiwa njiani kurejea nyumbani walishambuliwa na fisi eneo la vichaka ambapo alimng’ata Mwajuma sehemu za makalio na tumboni, hali iliyomlazimu Shija amsaidie huku akipiga kelele za kuomba msaada.

” wakati mwanaume huyo akitoa msaada kwa mpenzi wake, ndipo fisi alimng’ata usoni na ndipo aliposhindwa kutoa msaada na fisi huyo aliendelea kumshambulia mwanamke huyo hadi alipopoteza maisha papo hapo”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Willibrod Mutafungwa, alithibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo kwa kushambuliwa na fisi na kwamba fisi huyo aliuawa.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, majeruhi alikimbizwa Hospitali ya Rufani ya Nkinga ambako alilazwa na kutoa wito kwa wananchi mkoani Tabora kuwa makini na wanyama hatari kwa kutotembea usiku kwenye maeneo hatarishi kwa ajili ya usalama wao.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Maisha

Ajinyonga mpaka kufariki

Published

on

Joseph Ojur mwenye umri wa 52 mkazi wa ukanda wa  Kabagu katika manispaa ya Njeru amejinyonga mpaka kufa jumapili ya June 3 baada ya kunyimwaunyumba na mkewe.

Ojur inasemekana kuwa alimwambia mkewe kuwa alifanya vipimo vya ugonjwa wa UKIMWI na akakutwa nao.

Na tangu amwambie mkewe hivyo amekuwa akinyimwa ‘unyumba’.

Kamanda wa Polisi eneo la Njeru, Christopher Tuhunde amesema kuwa, marehemu alijinyonga ndani ya nyumba yake na jeshi hilo linaendelea kuchunguza kwa undani juu ya tukio hilo ili kuja na ripoti kamili kuhusiana na kujinyonga kwa Ojur.

Hata hivyo Tuhunde amewashauri wakazi wa eneo hilo kupenda kuomba ushauri kwa wenzao juu ya matatizo yanayowakabili kuliko kukimbilia kujiua.

Continue Reading

Maisha

Je, Unaweza Kujivunia Ujauzito ukiwa na umri gani? Brigitte Nielsen ametangaza kuwa Mjamzito

Published

on

Muigizaji nyota kutoka Italia ambaye ana asili ya Dernmark na aliyewahi kuwa mke wa zamani wa Sylvester Stallone ametangaza kuwa anatarajia kuwa ana ujauzito aliopewa na mume wake wa sasa Mattia Dessi.

Brigitte Nielsen ameshangaza wengi baada ya kutangaza ujauzito huo akiwa na umri wa miaka 54, na taarifa hizo amezitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Tayari ni mama wa watoto wanne ambao ni Julian, Killian, Douglas na Raoul ambaye ndio mtoto wake wa kwanza kwa mume wake wa sasa ambaye amedumu naye kwa miaka kumi na miwili tangu walipooana mwaka 2006.

happy time ❤ positive vibes #happyness #positivevibes

A post shared by Brigitte Nielsen (@realbrigittenielsen) on

Katika moja ya picha yake inayo onyesha tumbo la mtu mjamzito, aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya laki moja aliandika “Family is getting Longer” akimanisha kuwa sasa Familia inakua.

Mwanzoni amewahi kuwa kwenye ndoa na Roul Meyer, Sebastian Copeland, Sylvester Stallone na Kasper Winding.

Continue Reading

Maisha

Kenya: Mwanafunzi aunda gari linalotumia nishati ya jua Kenya

Published

on

Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ameunda gari linalotumia kawi ya jua, gari ambalo limekuwa likiwavutia watu sana mtaani kwake, na mtandaoni.

Samuel Karumbo, 30, ni mwanafunzi katika chuo cha mafunzo anuwai cha serikali mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya lakini ameliunda gari lake katika eneo la Langas, Eldoret si mbali sana na mji wa Kitale.

Anasema gari lake, ambalo lina mitambo mitatu ya sola iliyobandikwa, linaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 kwa siku.

Mitambo hiyo inaweza kuzalisha kadri ya jumla ya watu 260.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania