Connect with us

mahakamani

DODOMA: Jaji Mkuu Tanzania awataka watendaji wa Mahakama kufanya yafuatayo

Published

on

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewataka viongozi wa mahakama ikiwemo Naibu Wasajili, Mahakimu, Watendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo kutenda haki kwa watumishi walio chini yao.

Amesema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi wa mahakama Tanzania Mkoani.

“Sisi kama wasimamizi wakuu wa haki nchini tunawajibu mkuu wa kutenda haki kwa watumishi kwa vitendo, ni ukweli usiopingika kwamba kimbilio la mtumishi yeyote aliyepatwa na matatizo ni kwa kiongozi wake katika sehemu yake ya kazi, hivyo basi kila kiongozi anapaswa kufungua milango kwa watumishi waliopo chini yake” amesema Jaji Mkuu.

Aidha Jaji Mkuu amesema ubora wa viongozi unapimwa kwa namna wanavyosaidia wafanyakazi walio chini yao, na kuwataka viongozi hao kutokufunga milango yao kwa watumishi wanaowaongoza.

Mkutano huo wa Baraza la wafanyakazi wa Mahakama Tanzania umewashirikisha wajumbe kutoka kanda zote na menejimenti ya Mahakama Tanzania.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

mahakamani

Kesi ya Wema Sepetu yasogezwa mbele

Published

on

Msanii Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, ili kujitetea katika kesi yake kwa sababu amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Hayo yameelezwa na Mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali, Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani.

Wema Sepetu akiwa na Mama yake.

Wakili Kakula amedai kuwa anashangaa kutokumuona Wema, kwani hata ahirisho la mwisho la kesi yake hakuwepo.

Baada ha kueleza hayo, Mama Wema akatoa nyaraka za Wema za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Wakili Kakula amedai kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba mahakama isimamie sheria.

Mama Wema akiwa anaingia Mahakamani.

Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema ni kweli hakuna uthibitisho, hivyo katika tarehe ijayo uthibitisho unapaswa kuwepo, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi June 13,2018.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kuzitumia.

Inadaiwa Februari 4, 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February mosi 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Continue Reading

mahakamani

Tiptop Connection: Kesi ya babu tale, arejeshwa rumande tena kwa amri ya Mahakama

Published

on

Hukumu ya kesi inayomkabili Mkurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections na meneja wa msanii Diamond Platnumz, Hamis Shaban Taletale maarufu kama ‘Babu Tale’ na ndugu yake Iddi Shaban TaleTale iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016, iliwaamuru ndugu hao kumlipa fidia ya milioni 250, Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kwa makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila makubaliano naye.

Baada ya amri ya Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam, Babu Tale alitiwa mbaroni juzi na jana alipelekwa mahakamani hapo kwa ajili ya amri ya kumpeleka kifungoni.

Hata hivyo alilazimika kurudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi kwa kuwa Naibu Msajili, Wilbard Mashauri aliyetoa amri ya wawili hao kukamata hakuwepo.

Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Ruth Massam akatoa amri ya kurejeshwa rumande hadi hapo Naibu Msajili Mashauri aliyetoa amri ya kuwafunga atakaporejea kutoka Dodoma alikokwenda kikazi.

Continue Reading

mahakamani

MOI kumlipa Milioni 100 Aliyepasuliwa kichwa badala ya mguu

Published

on

Mahakama Kuu imeamuru Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu ya MOI kumlipa fidia ya Milioni 100 Emmanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu kutokana na madhara aliyoyapata ya kimwili na kiufahamu ikiwemo kupooza.

Mahakama imetoa amri hiyo baada ya Didas kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya taasisi hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2007 Didas alifanyiwa upasuaji wa kichwa alipofikishwa MOI badala ya mguu aliokuwa anaumwa.

Mgonjwa mwenzake, Emmanuel Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu ambao haukuwa na tatizo badala ya kichwa kutokana na makosa hayo, wagonjwa wote wawili walipelekwa katika hospitali ya Indraprastha Apollo, nchini India kwa matibabu zaidi hata hivyo, Mgaya alifariki dunia baadaye.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania