Connect with us

Burudani

Siri ya Dulla Makabila Kufungwa Jela

Published

on

Mwanamuziki wa Singeli nchini, Dullah Makabila amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa amekamatwa na jeshi la Polisi baada ya kumtia ujauzito mwanafunzi.
Akizungumza na kituo kimoja cha runinga Makabila amesema,  habari hizo si za kweli ila kuna watu wasiopenda mafanikio yake ndiyo wanasambaza taarifa mbaya kama hizo wakati siyo kweli na hana skendo kama hiyo.
“Taarifa hizo nimezipata wakati narudi kufanya show mkoani Iringa baada ya kupigiwa simu na meneja wa Diamond, Mkubwa Fella”
kuhusu habari hizo.

Msanii wa Muziki wa Singeli Dulla Makabila

Ikumbukwe kuwa kesi ya kumpa ujauzito mwanafunzi kwa mujibu wa sheria ya Tanzania ni kifungo cha miaka 30.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaoitwa ‘Kuingizwa’ ambao unafanya vizuri katika vituo vya radio nchini.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Burudani

Mlela ampasomo Diamond, amtaka kuwapiga chini warembo hawa

Published

on

Msani wa filamu Bongo, Yusuph Mlela amefunguka na kusema kuwa angekuwa yeye ndio Diamond Platinumz, basi asingekuwa na uhusiano na Zari, Hamisa Mobeto wala Wema Sepetu.

Staa huyo amesema hayo baada ya tetesi za mwanamuziki huyo kurudiana na mzazi mwenzake, Zari The Boss Lady.

Mlela amesema kuwa kwasababu Diamond ndiyo maisha aliyoyachagua basi hana budi kuendelea nayo kama alivyozolea.

Amesema kuwa Diamond ana maisha yake na maamuzi yake pia, kwa hiyo yeye afurahie tu maisha yake its ok, mimi siwezi kumpangia.

Pia amesema Ningekuwa mimi nisingekuwa nao wote (Zari, Mobeto wala Wema), siyo kwamba siwapendi, kwanza sitembei na watu maarufu ninatoka na watu wa kawaida tu,”.

Continue Reading

Burudani

Hii ndiyo sababu ya kifo cha Sam wa Ukweli

Published

on

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo imethibitishwa na msambazaji wa nyimbo zake ambaye pia Meneja wa ‘Team Mtaa kwa Mtaa’, Amri the Business aliyeeleza kwa masikitiko alivyopokea makubwa kuwa Sam amefariki dunia.

Msanii Sam wa Ukweli enzi za uhai wake.

Naye aliyekuwa mtayarishaji wa nyimbo za Sam wa Ukweli, Producer Steve amesema Sam alizidiwa zaidi Jumamosi iliyopita na walipomuuliza alisema ni ‘UKIMWI wa kulogwa’.

Sam wa Ukweli aliwahi kutamba na ngoma kama Sina Raha, Hata Kwetu Wapo, Kisiki, Milele na nyingine nyingi kali kuanzia mwaka 2010.

Baadhi ya mastaa walioumizwa na kifo cha msanii huyo na kuamua kutumia mitandao ya kijamii kuombeleza ni pamoja na Wolper.

Naye Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ameonyesha kuhuzunishwa na tukio la msio uliotokea wa msanii Sam wa Ukweli.

Continue Reading

Burudani

Sababu za Kim Kardashian kutokwa na machozi baada ya comment ya Kanye

Published

on

Siku za nyuma Kanye West alizua tafrani hasa kwa watu wenye asili ya Afrika baada ya kunukuliwa akisema kuwa watu weusi kuwa watumwa kwa miaka mia nne ilikuwa chaguo lao.

Kardashian anaendelea kusimama upande wa mume wake na anakubali kuwa maneno ya mume wake yalikuwa na story nyingine kabisa.

Anasema katika wimbo wenye Jina “wouldn’t Leave” ambao unapatikana katika album mpya ya “Ye” ndio unafafanua zaidi kile ambacho mume wake alikimaanisha pale aliposema utumwa ulikuwa kama chaguo.

Baadhi ya mistari iliyopo katika wimbo huo ni “Now I’m on fifty blogs gettin’ fifty calls / Wife calling screaming saying we’re about to lose it all. I had to calm her down cause she couldn’t breathe / I told her she could leave me now but she wouldn’t leave,”

Katika mahojiano aliyofanyiwa Kardashian wakati wa tuzo za mitindo za CFDA baada ya kupewa tuzo ya heshima ya mtu mwenye ushawishi alisema alilazimika kulia hasa baada ya kupigiwa simu na Kanye West akimueleza zaidi kuhusu maoni yake.

“Najua mume wangu alikuwa na nia njema, na nafahamu yeye atakuwa na nafasi nzuri ya kueleza zaidi kadiri  atakavyopata muda na nafasi nzuri” alisema Kim

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania