CWUR inapima ubora wa elimu na mafunzo kwa wanafunzi, ufahari wa wanafunzi walio katika vitivo mbalimbali pamoja na ubora wa tafiti bila kutegemea ‘data’ zilizokusanywa na chuo husika.
Kutoka bara la Afrika vyuo 14 tu vimeingia katika orodha ya vyuo 1000 bora Duniani kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Center for World University Rankings (CWUR) kwa mwaka huu 2018.
Ripoti hiyo imetaja idadi ya vyuo 7 Afrika Kusini, Misri(4), Nigeria(1), Tunisia(1) na Uganda(1) ndio vimeingia katika orodha ya vyuo 1000 bora Duniani.

Marekani ina jumla ya vyuo 8 katika Kumi bora, huku Chuo Kikuu Harvard kikishika namba 1 kwa mwaka wa 7 mfululizo sasa.
Chuo hicho kinafuatiwa na Chuo Kikuu cha Stanford, Chuo cha Ufundi Massachusetts, Chuo Kikuu cha Cambridge, Chuo Kikuu Oxford, Chuo Kikuu cha California, Berkeley, Chuo Kikuu Princeton, Chuo Kikuu Columbia, Chuo cha ufundi California na Chuo Kikuu cha Chicago.

Vyuo kutoka Afrika Kusini, Chuo Kikuu cha Cape Town kimeshika nafasi ya 223 huku ndio kikiwa Chuo cha kwanza Afrika, kimefuatiwa na Chuo Kikuu cha Witwatersrand(230), Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal(402), Chuo Kikuu cha Pretoria(438), Chuo Kikuu Stellenbosch(448), Chuo Kikuu cha Johannesburg(790) na Chuo Kikuu North-West(964).
Kutoka Misri, Chuo Kikuu Cairo kimeshika namba 452, kikifuatiwa na Chuo Kikuu Ain Shams(715), Chuo Kikuu Mansoura(884) na Chuo Kikuu Alexandria(903)
Chuo kutoka Uganda, Chuo Kikuu Makerere kimeshika nafasi ya 771, Chuo Kikuu Tunis El Manar kutoka Tunisia kimeshika nafasi ya 908 wakati Chuo cha Ibadan kutoka Nigeria kikishika nafasi ya 991.