Connect with us

Michezo

Mayweather ashika tena namba moja kwa Utajiri Duniani

Published

on

Bondia wa nchini Marekani, Floyd Mayweather ametwaa tena nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wanamichezo 100 matajiri zaidi duniani kwa mujibu wa Jarida la kibiashara la Forbes.

Bondia huyo alijipatia kitita cha Dola za kimarekani milioni 275 kufuatia ushindi wake katika pambano dhidi ya Conor McGregor, ambaye ameshika nafasi ya nne katika orodha hiyo.

LAS VEGAS, NV – AUGUST 10: Floyd Mayweather Jr. holds a media workout at the Mayweather Boxing Club on August 10, 2017 in Las Vegas, Nevada. Mayweather will face UFC lightweight champion Conor McGregor in a boxing match at T-Mobile Arena on August 26 in Las Vegas. (Photo by Isaac Brekken/Getty Images)

Mwanasoka nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye aliongoza orodha hiyo kwa miaka miwili mfululizo ameshuka hadi nafasi ya tatu akipigwa kikumbo na mpinzani wake wa Barcelona, Lionel Messi ambaye ameshika nafasi ya pili.

Katika orodha hiyo hakuna mwanamichezo mwanamke, baada ya mwanamkee pekee aliyekuwepo mwaka jana Serena Williams kuondolewa.

Wanamichezo hao 100 kwa ujumla wao walijipatia Dola za Kimarekani bilioni 3.8 likiwa ni ongezko la 23% kutoka mwaka jana limeeleza Jarida la Forbes, ambapo dereva wa mashindano ya Langalanga kutoka nchini Uingereza Lewis Hamilton akishika nafasi ya 12 na mapato ya dola milioni 51.

Hata hivyo wachezaji wa mpira wa kikapu wamedhibiti orodha hiyo kutokana na kulipwa mishahara minono iliyochochewa na mikataba kati ya Ligi ya NBA na makampuni ya Televisheni hasa matangazo yanayofikia dola bilioni 34.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Michezo

Siri ya Hazard kuisapoti Misri katika michuno ya Kombe la Dunia mwaka huu

Published

on

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Chelsea Eden Hazard amesema bila kupepesa maneno kuwa ataisapoti timu ya taifa ya Misri katika michuano ya Kombe la Dunia itakayo fanyika Urusi kuanzia mwezi huu.

Katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jana kati ya Misri na Ubelgiji, Misri ilikubali kichapo cha magoli matatu kwa nunge 3-0 ikicheza bila mshambuliaji wao nyota Mo Salah aliyepata majeraha ya bega wakati wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya 26 May.

Katika mahojiano baada ya kumalizika kwa mchezo huo Hazard alisema Misri ina wachezaji wazuri, na walifanikiwa kukabiliana nao na kupata ushindi hasa baada ya kupata goli la mapema.

Eden Hazard akiwa amevalia jezi ya timu yake ya taifa Ubelgiji

“Misri imebadilika sana kimchezo bila Salah na bado wamecheza vizuri na mtindo wao unafanana na ule wa timu ya taifa ya Tunisia” alisema Hazard

Hazard amesema alizungumza na Mo Salah baada ya kumalizika kwa Ligi ya mabingwa kwani ni rafiki yake sana na alimwambia anataka kumwona akicheza Kombe la Dunia.

“Nina matumaini kuwa Salah atarejea katika hali yake ya kawaida na atashiriki katika mashindao, nitafurahi kumuona na mimi nitashangilia Misri kwaajili yake.” alisema Hazard.

Wakati huo huo pia, wakala wa Mo Salah amekanusha tetesi kuwa Mchezaji wake atajiunga na miamba ya soka ya Hispania Barcelona.

Continue Reading

Michezo

Yanga: Fahamu kuhusu Mkataba mpya wa Hassan Kessy ndani ya Yanga

Published

on

Mkataba wa beki wa kulia wa klabu ya Yanga, Hassan Ramadhan Kessy unamalizika baadaye mwezi huu na taarifa zinasema mpaka sasa bado hajakaa na kufanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya ndani ya Klabu hiyo.

Akizungumza katika mahojiano hivi karibuni mara tuu baada ya Yanga kutupwa nje ya mashindao ya SportPesa Cup huko Nakuru Kenya licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika mashindano hayo, Kessy amekiri kuwa mpaka sasa bado hajajua hatma yake ndani ya klabu ya Yanga juu ya kutia saini mkataba mpya.

Hassan kessy aakiwa amevalia Jezi nyekundu ya Simba

“Mpaka sasa hatujafanya mazungumzo yoyote, nakwenda kupumzika kwanza, mambo ya mkataba mpya nimemwachia msimamizi wangu” alisema Kessy.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema klabu hiyo itawabakiza nyota wote ambao Kocha Mkuu Mwinyi Zahera amependekeza wabaki licha ya kugoma kuwataja majina.

Hassan Kessy alijiunga na Yanga akitokea Simba mwaka 2o16 huku uhamisho wake ukigubikwa na misukosuko.

Continue Reading

Michezo

CECAFA: Simba na Yanga zakutana kundi moja, Kukipiga tena tarehe 5 July

Published

on

Kuelekea Michuano ya CECAFA Kagame Cup klabu za samba na Yanga za jijini Dar es salama zimewekwa katika Kundi moja.

Katika mkutano na wanahabari, Katibu mkuu wa CECAFA Bw. Nicholas Musonye, amesema mashindano ya mwaka huu yataanza tarehe 28 Juni, 2018 na kumalizika tarehe 13 Julai 2018.

“Tumezingatia ratiba ya Kombe la Dunia, hivyo mechi hizi hazitaingiliana na ratiba ya Kombe la Dunia” amesema Musonye.

Kwa upande wake rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Walis Karia amesema kuanzia sasa wanajipanga ili mashindano haya yawe yanafanyika kila mwaka yasiwe yanasimama simama.

Simba na Yanga ziko Katika Kundi C ambapo kuna timu kama St. George kutoka Ethiopia na Dakadaha kutoka Somalia.

Kundi B kuna timu ya Rayon kutoka Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Ports ya Djiboud na Lydia ya Burundi.

Katika Kundi A la Michuano ya CECAFA mwaka huu kuna timu ya Azam FC kutoka Tanzania Bara, JKU ya visiwani Zanzibar, Kator na Ugazote zikiwa ni kutoka Uganda.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania