Connect with us

Siasa

Mrema aeleza sababu za kutojiunga na UKAWA na amtaja mrithi wake ndani ya TLP

Published

on

Mwenyekiti wa chama cha TLP Tanzania Labour Part, Augustino Liatonga Mrema amesema hawezi kujiunga na UKAWA kutokana na kile anachodai kuwa sera zao ni kuandaa matukio ya kumdhalilisha rais.

Akizungumza katika mahojiaano na moja ya radio nchini hii leo June 7, Mrema amesema UKAWA wangekuwa na nia ya dhati basi Profesa Lipumba asingeondoka katika Umoja huo.

“Badala ya wao kukazania majimbo mengine huko wao wakaja Vunjo kunitoa mimi wakiniona kama mpinzani wao mkubwa” alisema Mrema.

Mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema (kushoto) akiwa na Mbunge wa Vunjo James Mbatia (kulia)

Mrema ameeleza kilichosababisha asipate ushindi katika Jimbo la Vunjo ni Propaganda za wapinzani wake ambao awali walimfata na kumueleza mengi hasa juu ya afya yake na walimwambia kuwa yeye ni marehemu mtarajiwa.

“Kwakweli hali yangu haikuwa nzuri kiafya lakini bado nilikuwa naweza kufanya kazi, wakamchagua mwenzangu, sasa hivi nimepona” alisema Mrema.

Akitolea ufafanuzi juu ya matukio ambayo upinzani wanatengeneza, amesema mfano lile tukio la Mh. Mkapa kwamba amekula milioni 900, wao walilitengeneza ili kumnyima sifa kwa wananchi na wawamini wao na kuwapatia nafasi.

“Tulilitengeneza sisi ili tujipatie umaarufu ila haikuwa kweli” alisema Mrema.

Kuhusu nafasi yake uenyekiti ndani ya chama amesema sio kama nang’ang’ania madaraka ya Uenyekiti wa TLP bali amefanikiwa kumpata kijana mwenye ubora atakayeweza kufanya kazi vizuri.

“Mimi sina haja ya kuendelea, namuachia, lakini vijana hawataki kuongoza kwenye hivi vyama ambavyo havina hela” alisema Mrema.

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Siasa

Gina Haspel, Mwanamke wa kwanza Kuteuliwa kuwa CIA Marekani

Published

on

Seneti ya Marekani imeidhinisha uteuzi wa Gina Haspel kama mkurugenzi na mwanamke wa kwanza wa CIA, huku akipigiwa kura na maseneta 54 kwa kura ya ndiyo wakati 45 wakipiga kura ya hapana.

Haspel, ambaye ni mkongwe katika shirika la ujasusi la Marekani, CIA, alikabiliwa na upinzani mkali wakati wa kunadiwa kwake kutokana na nasaba yake na CIA pamoja na mbinu zake za namna ya kuhoji watuhumiwa zilivyokuwa za kipekee.

Inaelezwa kuwa, Gina awali alikuwa msimamizi wa gereza moja la siri ambalo liko nje ya Marekani ambako watuhumiwa wa ugaidi walikuwa chini ya bweni la maji, ambapo mateso waliyokuwa wakiyapata ni kuzamishwa katika kina cha maji adhabu ambayo wengi huona ni mateso makubwa.

John McCain, Seneta wa chama cha Republican ni miongoni mwa watu waliokumbana na mateso ya namna hiyo alipokuwa akiteswa kwenye jela mojawapo nchini Vietnam kwa miaka mitano na alipopata fununu za kuteuliwa kwa Gina alipinga bila wasiwasi.

Mnamo mwaka wa 2002 Haspel alichaguliwa na shirika hilo kuongoza kitengo kilichoitwa “black site” huko nchini Thailand mahali ambako mbinu za mahojiano ya kikatili zilitekelezwa, na ripoti ya seneti ikaita mbinu hizo kuwa ni mateso.

Kwa sasa Bi Haspel amesema CIA haipaswi kutumia tena mbinu za namna hiyo.

Hata hivyo inaarifiwa kuwa raisi Trump amesema Marekani itaendelea na mbinu hizo hizo za kumfunga mtuhumiwa wa ugaidi kitambaa usoni, akiwa amelala kwenye ubao na kutupwa kwa kasi kwenye kina cha maji huku mtu huyo akiwa ametanguliza kichwa

 

Continue Reading

Siasa

Dodoma: Serikali yabainisha idadi ya sheria zilizoridhiwa na Bunge la Afrika Mashariki

Published

on

Serikali imebainisha jumla ya sheria 78 zimetungwa tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika mashariki hadi sasa na kati ya hizo 20 tayari zimeridhiwa na Wakuu wa nchi wanachama na zingine bado zipo kwenye hatua mbalimbali za kusainiwa na kuridhiwa.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga ameyasema hayo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Malindi Mh. Ally Salehe aliyehitaji kufahamu idadi ya sheria zilizotungwa tangu kuanzishwa kwake.

Balozi Dkt. Mahiga amesema sheria zilizotungwa na Bunge la Afrika Mashariki zimelenga kuimarisha biashara, kukuza uchumi  wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwezesha taasisi na vyombo vyake kuweza kutekeleza majukumu yake.

Bunge la Afrika Mashariki lilianzishwa mwaka 2001 na linajumuisha wabunge wa nchi zote wanachama.

 

Continue Reading

Siasa

Zitto atoa yake Ziara ya kushtukiza iliyofanywa na rais Bandarini

Published

on

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema ziara ya iliyofanywa na Rais Magufuli katika Bandari ya Dar es Salaam sio suluhisho bali suluhisho la kudumu ni kutekeleza Mkakati wa Mkoa wa Kigoma wa kulima Hekta 100,000 za michikichi na kilimo cha Alizeti ili Tanzania ijitosheleze na kuuza nje mafuta ya kula.

“Elekeza hayo kwa Mawaziri wa Kilimo, Fedha na Viwanda” ameandika Zitto Kabwe.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania