Connect with us

Uncategorized

Kenya: Wavuvi 109 raia wa Tanzania wakamatwa

Published

on

Jeshi la majini nchini Kenya limewakamata wavuvi 109 raia wa Tanzania kwa kosa la kufanya shughuli za uvuvi kwenye mipaka ya Kenya katika bahari ya Hindi kinyume na sheria.

Wavuvi hao walikamatwa katika kijiji cha Shimoni kilichopo kusini mwa Kenya karibu na mpaka wa Tanzania na kufikishwa katika mahakama ya Kwale June 3.

Aidha wavuvi hao walishindwa kujiwekea dhamana ya zaidi ya shilingi laki nne za kitanzania  kwa kila mmoja.

Kwa upande mwingine Mbunge wa Lunga Lunga, Khatibu Mwashetani amewateteta wavuvi hao na kuomba makamu wa rais  wa Kenya Ruto kuingilia sakata hilo ili kuzuia mgogoro wa kidiplomasia unaoweza kutokea.

Na mbunge huyo aliongeza kwa kusema kuwa wavuvi hao ni kama ndugu zao kwa sababu wanashirikiana katika mambo mengi

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Uncategorized

Ujerumani: Leroy Sane akunana na Panga la Joachim Low, atemwa dakika za mwisho

Published

on

Winga wa Manchester City Leroy Sane ameachwa nje ya kikosi cha mwisho cha Ujerumani kitawakilisha mabingwa hao watetezi Kombe la Dunia baadaye mwezi huu baada ya kocha wa timu hiyo Joachim Low kupunguza wachezaji kutoka 27 hadi 23.

Sane amekuwa na mafanikio sana akichezea Manchester City kiasi kwamba alitawazwa mchezaji bora chipukizi wa mwaka  katika ligi ya Premia, alifungia City magoli 14 na kusaidia ufungaji wa mabao mengine 19.

Wachezaji wengine waliopunguzwa ni pamoja na wachezaji wa Bayer Leverkusen Bernd Leno na Jonathan Tah na mshambuliaji wa Freiburg Nils Petersen.

Kipa Manuel Neuer, aliyerejea kucheza baada ya kukaa nje miezi tisa wakati wa mechi ambayo walilazwa na Austria 2-1 Jumamosi, yumo kwenye kikosi.

Ujerumani wamo Kundi F na Mexico, Sweden na Korea Kusini, na watacheza mechi yao ya kwanza mnamo Jumapili 17 Juni.

Kikosi Cha Ujerumani kinaundwa na wachezaji wafuatao.

Walinda lango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre ter Stegen (Barcelona), Kevin Trapp (Paris St-Germain)

Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Matthias Ginter (Borussia Monchengladbach), Jonas Hector (Cologne), Mats Hummels (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich), Marvin Plattenhardt (Hertha Berlin), Antonio Rudiger (Chelsea), Niklas Sule (Bayern Munich)

Viungo wa kati: Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Paris St-Germain), Leon Goretska (Schalke), Ilkay Gundogan (Manchester City), Sami Khedira (Juventus), Toni Kroos (Real Madrid), Mesut Ozil (Arsenal), Sebastian Rudy (Bayern Munich)

Washambuliaji: Mario Gomez (Stuttgart), Thomas Muller (Bayern Munich), Marco Reus (Borussia Dortmund), Timo Werner (RB Leipzig)

 

Continue Reading

Uncategorized

Masau Bwire alivyokuwa Mzee wa busara kwa Yanga, aandika ujumbe huu

Published

on

Shida haina adabu, inadhalilisha, inaudhi, inakosesha furaha, amani, inakuondolea thamani na utu kwa watu, shida ni kitu kibaya mno, usiombe ikutokee, wala usimcheke mwenye shida maana ipo siku, itahamia kwako, utajuta kuzaliwa, haina adabu hii, leo kwake, kesho kwako, hivyo, tusichekane wakati wa shida, tuhurumiane na kufarijiana sisi kwa sisi.

Wakati wa shida utamjua ndugu, rafiki wa kweli, utamjua mnafiki, ambaye shida ikikutokea anakataa undugu, siyo rafiki yako tena, kutwa kukusimanga tu kwa watu, shida wakati fulani ni makusudi ya Mungu kutaka ujue utu wa watu kwako, lakini pia shida ni kipimo kinachokuonesha ndugu na rafiki wa kweli, wanafiki utawajua wakati wa shida!

Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire

Hakuna wakati unaohitaji uvumilivu, ‘kuziba masikio’, ushirikiano na mshikamano kama wakati wa shida, ni hivi tu vitakuondolea shida inayokutesa kwa wakati wako, shida haikimbiwi, inakabiliwa, tena ikikabiliwa kwa pamoja, itatoweka haraka, hali ya kawaida itarudi, tena kwa ufanisi mkubwa pengine kuliko mafanikio kabla ya shida hii!

Ndugu zangu, rafiki zangu wana wa Jangwani, Young Africans, poleni sana, mpo kwenye kipindi kigumu sana, kipindi cha shida kubwa, kipindi ambacho mnatakiwa msimame imara sana kukabiliana na shida hii ili iondoke, ni cha mpito tu, Mungu ni wa wote, mkipambana, atawaonesha njia ya kutokea, mambo yatakuwa mwemwelemwemwele, mtafanikiwa sana!

Ushauri wangu kwenu, shikamaneni, msinyosheane vidole, msilaumiane wala kutafutana uchawi, kuweni kitu kimoja, mjadili, mshauriane kwa pamoja, kamwe msikimbiane, simameni imara muikabili hali hii kwa pamoja.

Nimesema awali, shida ni kipimo cha utu wa mtu, kukuonesha ndugu, rafiki wa kweli na wanafiki, wanaokukimbieni wakati huu wa shida, hao Mungu anakuonesheni kwamba, siyo wote waliomo katika zizi ni wa zizi hili, waacheni waende maana mlikuwa nao zizini kumbe hawakuwa wa zizi hili!

Kwa niaba ya Ruvu Shooting, tunawaombea kwa Mungu, kwa moyo wa upendo na wa dhati kabisa shida hii inayotokana na ukata, iwaondoke kabla ya msimu mpya wa ligi 2018/19, mpate mahela mengi, muwe katika hali yenu ya miaka ya nyuma, umataifa wenu uonekane, tena kwa kasi, sisi hatuwaombei njaa, tunawaombea mafanikio ili tuwapapase maana, msimu uliomalizika 2017/18 tuliwahurumia kuwapapasa kutokana na shida mlionayo tukitekeleza agizo la Mungu, “Hurumianeni, farijianeni ninyi kwa ninyi”.

Continue Reading

Uncategorized

Shilole “Watoto wangu nawalea katika maadili siwezi kuwalea kistaa”

Published

on

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amesema mavazi anayovaa kwenye shoo au sehemu mbalimbali za starehe hayupo tayari kuwaona watoto wake wakiiga.

Staa huyo amedai kuwa watoto wake wanatakiwa kujua kuwa mama yao yupo kazini na si aina ya mavazi anayopenda kuyavaa.

Msanii Shilole.

 

Shilole akiwa na mabinti zake.

Amesema kuwa “Watoto wangu nawalea katika maadili siwezi kuwalea maisha ya kistaa kama ambayo mimi nayafanya, mavazi ninayovaa sehemu mbalimbali ni kutokana na kazi yangu na wanalijua hilo.

Pia amesema kuwa watoto wake hawana dalili za kuja kuwa mastaa, hivyo lazima wakae mbali na aina hiyo ya mavazi kwa kuwa wanalelewa mazingira ya dini,”.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2018 HELLO Media Tanzania